Wednesday, May 9, 2012

BAADHI YA MIUJIZA ILIYOTENDEKA KATIKA MIKUTANO YA AFRIKA KUMEPAMBAZUKA NCHINI MSUMBIJI

Mnamo mwaka jana mwezi wa pili AFRIKA KUMEPAMBAZUKA ilifanya uzinduzi maalum wa mwaka wa uamsho katika bara la afrika, uzinduzi huo lifanyika pale katika viwanja vya jangwani na baada ya uzinduzi uo afrika kumepambazuka ilifika katika nchi ya msumbiji china ya mkurugenzi wake mch.MOSES MAGEMBE na kuzunguka majimbo7 kati ya 10 yaliyopo nchini humo. miujiza mingi mikubwa ilifanyika na watu wengi walimgeukua mungu.

PICHA ZA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA NAMPULA NA PEMBA
(NAMPULA) ndugu huyu alifika mkutanoni akiwa ni mgonjwa na pia hawezi kutembea

Mchungaji Magembe alichukua magongo na kuanza kumuombea apate uponyaji

Baada ya maombi ndugu kuulizwa anajisikiaje akasema amepona mchungaji Magembe akiwa ameinua gongo kumshangilia mungu kwa matendo yake makuu

Ndugu huyu aliambiwa atembee ili kudhihilisha uponyaji ulio fanyika ndani yake

Rafiki yangu alitembea na kukimbia kabisaa.. mpaka watu wakabaki wana mshangaa mungu anavyotenda mambo makubwa



Pia mama huyu alifika mkutanoni akiwa hawezi kutembea ameletwa kabebwa rakini baada ya maombi aliweza kusimama na kukimbia

Ndugu huyu pia alifika akiwa hawezi kutembe, akitembea kwa msaada wa gongo,
( mchugaji magembe alimuombea)

Ndugu huyu alipokea uponyaji na kuanza kutembea

Katika nchi ya msumbiji mikutano ya injili imekua ikifanyika mida ya jioni kuanzia saa12-2usiku na watu wengi wamekua wakiokolewa na kuponywa



( PEMBA) Umati wa watu waliokubali kumpa yesu maisha yao katika mkutano wa jimbo la pemba nchini msumbiji



(NAMPULA) watu waliofika na kukaa kulisikiliza neno la mungu katika jimbo la nampula nchini msumbiji na wengi mpaka jengo pamoja na viti vikawa havitoshi ikabidi wengine wajikalie chini ili waweze kulisikiliza neno la mungu

Watoto hawa nao wanaliitaji neno mpaka wakakubali kukaa chini wamsikilize muhubiri

watu woote wakiwa makini kulisikiliza neno la mungu

Baada ya neno nguvu za mungu kwa wingi zilishuka na kuanza kuhusika na maisha ya watu

Wababa hawa wameguswa na nguvu nyingi za mungu na wamejimimina kwa mungu

1 comment:

  1. KARIBU GOSPEL CAMPAIGN CENTRE T.A.G MAJUMBA SITA UMPE YESU MAISHA YAKO NA PATE UPONYAJI WAKO LEO

    ReplyDelete