- utumiaji wa mafuta ya upako
- utumiaji wa vitambaa
- utumiaji wa maji yanayoitwa yamebarikiwa
- utumiaji wa maua ya baraka
na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikitolewa na wahubiri mbalimbali wengi wao kwa makusudi na baadhi yao kwa kuto kujua au kukosa mafundisho sahihi, hivyo Mch Magembe ametangaza kuwa operation hiyo sasa itaendelea kwa miezi mitatu mfululizo yaani mwezi wa kumi, wakumi na moja, na wakumi na mbili. Akiendelea kufundisha katika operation hiyo, Mch Magembe alisisitaza kuwa wahubiri wote wa kikristo wanao tumia vitu hivyo waache mala moja kwani hakuna msaada wowote katika vitu hivyo na pia biblia haijatuagiza hivyo ila biblia imeagiza kulitumia JINA LA YESU pekee kwani kwa JINA LA YESU hakuna kinacho shindika na jina hilo ndilo jina pekee litupasalo wanadamu wote kuokolewa kwalo kutoka katika vifungo vya mwovu shetani.
Operation ikiendelea katika ibada iliyofanyika tareh 23/9, mchungaji moses magmbe akiongoza maombezi kwa watu waliofika kuhitaji maombezi na kufunguliwa.
Baadhi ya wahudum wa kanisa la majumba sita wakitoa huduma kwa mojawapo ya watu waliofika katika ibada hiyo
Umati wa watu wakiendelea na maombezi katika ibada hiyo
No comments:
Post a Comment