Tuesday, May 8, 2012

IBADA KUBWA ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MAJUMBA-SITA JUMAAPILI HIHI

Baada ya ubatizo ulio fanyika katika kanisa la majumbasita, wikii yote kulkua na semina iliyokua ikiendeshwa na mtumishi wa mungu mmishenali Saju mathew. kutoka India, fuatilia pamoja nami matukio mbalimbli katika ibada hiyo.

washirika wa kanisa la majumbasita wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikiongelewa madhabauni  baada ya mchungaji Magembe kusimama.

Familia hii ilipokelewa rasmi katia ibada hiyo na kutambulishwa na mchungaji Magembe kama washirika wapya katika kanisa la majumbasita.



baadhi ya wazee wa kanisa wakipeana mikono na wageni hao mara baada ya kutambulushwa na kukaribishwa na mchugaji.

Kulia ni mmishenari Saju wa kutoka India akiwa pamoja na mzee kiongozi(mr.Hezron nyagawa) wa kanis la T.A.G. M/6 wakifuatilia kwa makini kilichokua kikiendelea ibadani.

Mchungaji Moses Magembe(kushoto) akizungumzia huduma ya mmishenari Saju pamoj na kumshukuru kwa semina iliyokuwa ikiendelea wikizima lililopita, pia kwa kumleta mkewake Tanzania ambaye washirika wote wa m/6 walikua na hamu kubwa ya kumuona.( katikati ni mama Saju na mwishoni kulia ni mmishenari Saju).


Pia mama Saju alipata nafasi ya kuzungumza na kuliaga kanisa
(mchungaji magembe akimsikiliza kwa makini kwaajili ya kutafsiri )

Pia mchungaji Saju alipata nafasi yya kuliaga kanisa na kuhitimisha semina kwa neno la mungu. (mch.Magembe  akitafiri)




Picha na Yohana Magembe.




1 comment: