Wednesday, May 9, 2012

BAADHI YA MIUJIZA ILIYOTENDEKA KATIKA MIKUTANO YA AFRIKA KUMEPAMBAZUKA NCHINI MSUMBIJI

Mnamo mwaka jana mwezi wa pili AFRIKA KUMEPAMBAZUKA ilifanya uzinduzi maalum wa mwaka wa uamsho katika bara la afrika, uzinduzi huo lifanyika pale katika viwanja vya jangwani na baada ya uzinduzi uo afrika kumepambazuka ilifika katika nchi ya msumbiji china ya mkurugenzi wake mch.MOSES MAGEMBE na kuzunguka majimbo7 kati ya 10 yaliyopo nchini humo. miujiza mingi mikubwa ilifanyika na watu wengi walimgeukua mungu.

PICHA ZA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA NAMPULA NA PEMBA
(NAMPULA) ndugu huyu alifika mkutanoni akiwa ni mgonjwa na pia hawezi kutembea

Mchungaji Magembe alichukua magongo na kuanza kumuombea apate uponyaji

Baada ya maombi ndugu kuulizwa anajisikiaje akasema amepona mchungaji Magembe akiwa ameinua gongo kumshangilia mungu kwa matendo yake makuu

Ndugu huyu aliambiwa atembee ili kudhihilisha uponyaji ulio fanyika ndani yake

Rafiki yangu alitembea na kukimbia kabisaa.. mpaka watu wakabaki wana mshangaa mungu anavyotenda mambo makubwa

Tuesday, May 8, 2012

IBADA KUBWA ILIYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MAJUMBA-SITA JUMAAPILI HIHI

Baada ya ubatizo ulio fanyika katika kanisa la majumbasita, wikii yote kulkua na semina iliyokua ikiendeshwa na mtumishi wa mungu mmishenali Saju mathew. kutoka India, fuatilia pamoja nami matukio mbalimbli katika ibada hiyo.

washirika wa kanisa la majumbasita wakisikiliza kwa makini kilichokuwa kikiongelewa madhabauni  baada ya mchungaji Magembe kusimama.

Familia hii ilipokelewa rasmi katia ibada hiyo na kutambulishwa na mchungaji Magembe kama washirika wapya katika kanisa la majumbasita.