Sunday, October 21, 2012

Baada ya kuona uhitaji mchunga atangaza operation iliyokuwa ya wiki tano kuendelea kwa miezi mitatu mfululizo.

Baada ya kuendesha operation ya wiki tano mfululizo juu ya uponyaji kwa njia za kibiblia, mchungaji kiongozi wa kanisa la GOSPEL CAMPAIGN CENTRE (T.A.G MAJUMBA SITA) lililopo ukonga jijini dar es salaam, Mchungaji Moses Magembe amesema ameona uhitaji mkubwa sana uliopo na jinsi watu wanavyo teswa kwa njia mbalimbali za maombezi zisizokuwa za kibiblia zilizo ingizwa kanisani na kikundi cha watu wanao jiita kuwa ni watumishi wa mungu huku wakitumia biblia kuwalaghai watu kwa injili isiyokuwa sahihi na kufanya maombezi kwanjia mbalimbali ambazo siyo za kibiblia ikiwemo



  • utumiaji wa mafuta ya upako
  • utumiaji wa vitambaa
  • utumiaji wa maji yanayoitwa yamebarikiwa
  • utumiaji wa maua ya baraka

na vingine vingi ambavyo vimekuwa vikitolewa na wahubiri mbalimbali wengi wao kwa makusudi na baadhi yao kwa kuto kujua au kukosa mafundisho sahihi, hivyo Mch Magembe ametangaza kuwa operation hiyo sasa itaendelea kwa miezi mitatu mfululizo yaani mwezi wa kumi, wakumi na moja, na wakumi na mbili. Akiendelea kufundisha katika operation hiyo, Mch Magembe alisisitaza kuwa wahubiri wote wa kikristo wanao tumia vitu hivyo waache mala moja kwani hakuna msaada wowote katika vitu hivyo na pia biblia haijatuagiza hivyo ila biblia imeagiza kulitumia JINA LA YESU pekee kwani kwa JINA LA YESU hakuna kinacho shindika na jina hilo ndilo jina pekee litupasalo wanadamu wote kuokolewa kwalo kutoka katika vifungo vya mwovu shetani.
Operation ikiendelea katika ibada iliyofanyika tareh 23/9, mchungaji moses magmbe akiongoza maombezi kwa watu waliofika kuhitaji maombezi na kufunguliwa.
Baadhi ya wahudum wa kanisa la majumba sita wakitoa huduma kwa mojawapo ya watu waliofika katika ibada hiyo

Umati wa watu wakiendelea na maombezi katika ibada hiyo








Sunday, August 26, 2012

Mchungaji Azindua Operation maalum ya wiki tano ya maombezi na uponyaji

Ø Asema sasa ameamua kutangaza mpango kabambe wa kuwafungua watu
Ø Asema  kuna kikundi cha wahuni 
kimejipenyeza  kuadaa ulimwengu
 Ø Waliodanganywa na kupewa vitambaa,   
      vyungu,  mafuta wavisalimisha.


Mchungaji kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign Centre, la Majumbasita UkongaJijijini Dar es salaam, 
 Moses Magembe, amezindua kampeni maalumu ya maombi na maombezi, kwa muda wa majuma matano, ambapo kazi ya kuwafungua na uponyaji unaoambatana na matendo makuu ya nguvu za Mungu  utaanza rasmi.                                                                     
Akiongea katika Ibada ya  hiyo maalum alisema  kazi ambayo ameianza haitazimwa bali ameamua kuwasha moto katika siku za Jumatano,Alhamisi,Ijumaa na Jumapili kwa muda wa majuma yote matano fulululizo, hivyo ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na Vitongoji vyake, wakiwepo watu kutoka mikoa mbalimbali, kujitokeza kwa wingi kuhudhuria maombezi hayo muhimu kwani katika kanisa hilo, masuala ya miujiza siyo kitu cha kushangaza bali watu wamekuwa wakitendewa na Mungu pasipo shaka.                                                                     

Akitoa mfano alianza kwakuwainua makundi mbalimbali  ya watu ambao wametendewa miujiza na walioponywa ukimwi na kuthibitishwa na madaktari ,wakifuatiwa na kundi lingine la watu waliokuwa wakiteswa na vifafa, waliokuwa hawapati watoto na wale ambao wamebarikiwa Baraka mbalimbali, zikiwepo kujenga nyumba,mashamba,magari n.k, mkundi yote hayo yaliweza kusimama nkudhihirisha kuwa hakika 
Mungu amewatendea. Huku akisimamia somo lake la Jina la Yesu ni jina la Pekee, huku akikemea mfumo wa kanisa kugeuka kuwa kibanda cha Waganga wa kienyeji kwa kutumia mifumo ya kuwapaka watu mafuta na wengine kuyauza kwa gaharama kubwa, jambo ambalo alisema kuwa ni upotofu wa hali ya juu wa kiimani, kwani jina la Yesu halihitaji msaada kwani msaada ni Roho mtakatifu pekee na si njia za ujanja ujanja za unaofanywa na waganga wa kienyeji. Akiongea kwa upako wa aina yake uliojaa nguvu za Mungu, Mchungaji Magembe alisema Jina la Yesu, halijafilisika kiasi cha kuhitaji msaada wa mafuta,chungu,fruto, wala kibakuli kwani jina hilo limemwaga damu mara moja na linauwezo wa kuwaweka watu huru pasipo mazingaombwe yoyote.   

Kinachotakiwa madhabahuni ni Biblia tu, na wala sio ujanja wa kugeuza Black Curent, eti damu  ya Yesu, ambao alisema kuwa  huo ni ujanja wala sio kweli kwani, watu wamefundishwa vibaya na wamekuwa wakielekezwa kama waganga wa kienyeji wanavyofanya kwa wateja wao kwa kuwalazimisha watu kutembea na mafuta,chumvi,na makorokoro mengine.
Katika ibada hiyo ya kipekee, Mchungaji Magembe alifundisha na kuwaelekeza watu kweli ya Mungu, ambapo watu wengi walikuwa wamesalimisha vitambaa,chumvi,mafuta,chungu,shanga na makolokolo mengine ambayo walikuwa wamepewa na wahubiri yakiwepo maua ya Baraka.


Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Gospel Campaign, Majumbasita Ukonga, jijini Dar es Salaam na Mchungaji msaidizi wa Kanisa hilo, Hilda Magembe wakiwa Ibadani.( Picha Zote na J&M WAMOJA BLOG)

Wafanyakazi wa Wapo Radio nao walikuwepo kwenye mkakati huo maalum

Watu wengi walifunguliwa kupitia Ibada hiyo ya kipekee mara baada ya kuombewa na mpakwa mafuta wa huyo wa Bwana, Mchungaji Moses Magembe ambaye ameamua kujitoa mhanga, kuieleza kweli mbele ya jamii ya Wakristo, na kuipinga imani potofu zilizozagaa nchini, huku akiamua kuendesha Operation maalumu, ya maombezi kupitia jina kuu la BWANA Yesu Kristo. 

Wednesday, May 9, 2012

BAADHI YA MIUJIZA ILIYOTENDEKA KATIKA MIKUTANO YA AFRIKA KUMEPAMBAZUKA NCHINI MSUMBIJI

Mnamo mwaka jana mwezi wa pili AFRIKA KUMEPAMBAZUKA ilifanya uzinduzi maalum wa mwaka wa uamsho katika bara la afrika, uzinduzi huo lifanyika pale katika viwanja vya jangwani na baada ya uzinduzi uo afrika kumepambazuka ilifika katika nchi ya msumbiji china ya mkurugenzi wake mch.MOSES MAGEMBE na kuzunguka majimbo7 kati ya 10 yaliyopo nchini humo. miujiza mingi mikubwa ilifanyika na watu wengi walimgeukua mungu.

PICHA ZA MIKUTANO KATIKA JIMBO LA NAMPULA NA PEMBA
(NAMPULA) ndugu huyu alifika mkutanoni akiwa ni mgonjwa na pia hawezi kutembea

Mchungaji Magembe alichukua magongo na kuanza kumuombea apate uponyaji

Baada ya maombi ndugu kuulizwa anajisikiaje akasema amepona mchungaji Magembe akiwa ameinua gongo kumshangilia mungu kwa matendo yake makuu

Ndugu huyu aliambiwa atembee ili kudhihilisha uponyaji ulio fanyika ndani yake

Rafiki yangu alitembea na kukimbia kabisaa.. mpaka watu wakabaki wana mshangaa mungu anavyotenda mambo makubwa